Serikali kwa
kushirikiana na wadau wameandaa mapendekezo ya Sheria ya Usalama wa Barabarani
sura 168 ambapo pamoja na mambo mengine inalenga kuzuia matumizi mabaya ya simu
wakati dereva anapoendesha gari.
Akiwasilisha
bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2018/19, Waziri wa Mambo ya Ndani Dk Mwigulu
Nchemba amesema pendekezo jingine ni kuondoa nukta kwenye leseni za madereva
wanaokiuka Sheria za usalama wa barabarani
Dk Mwigulu
amesema hali ya usalama wa barabarani imeendelea kuimarika kutokana na hatua za
kisheria zinazochukiliwa kwa madereva na wamiliki wa vyombo vya moto
Amesema katika
kipindi cha Julai mwaka 2017 hadi Machi mwaka 2018 jumla ya ajali 4180 za
barabarani ziliripotiwa na kwamba ajali 1613 zilisababusha vifo vya watu 1985
na watu 4447 kujeruhiwa
" Takwimu
zinaonyesha kupungua kwa ajali za barabarani kwa asilimia 35.7ikilinganishwa na
kipindi kama hicho mwaka 2016/17," amesema.
Matumizi ya simu kwa madereva yaundiwa sheria
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment