Maaskofu wote 34 wa Kanisa Katoliki
nchini Chile wamemuomba Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis
aridhie kujiuzulu kwao kutokana na kashfa ya udhalilishaji kingono iliyolikumba
Kanisa hilo nchini humo.
Maaskofu hao wanatuhumiwa kwa kuzuia
uchunguzi wa kashfa ya ngono inayomuhusu Kasisi mmoja anayetuhumiwa kwa
kumlawiti mtoto mdogo wa kiume.
Kashfa hiyo inamhusu Askofu Juan
Barros ambaye anatuhumiwa kutumia wadhifa wake ndani ya Kanisa Katoliki
kujaribu kuzuia uchunguzi dhidi ya tuhuma za udhalilishaji kingono
zinazomkabili Kasisi Fernando Karadima.
Maaskofu hao wameomba msamaha kwa waathirika
na Kanisa kwa ujumla kwa makosa hayo makubwa na uzembe. Hata hivyo mpaka sasa
haijafahamika kama Papa Francis ameridhia ombi la Maaskofu hao kujiuzulu.
Maaskofu 34 katoliki waomba kujiuzulu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 18, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment