Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul
Makonda, ameunda kamati ya watu 18 kutoka makundi mbalimbali ya jamii wakiwemo
wanaharakati na wanasheria wa kutetea haki za watoto na wanawake kwa ajili ya
kutatua tatizo la ongezeko la watoto wa mitaani.
Akizungumza Jijini Dar es salaam,
Mh. Makonda ameipa kamati hiyo mwezi mmoja ili kuja na njia zinazopaswa
kutumika kudhibiti tatizo hilo ambapo amesema, utafiti uliofanywa na Idara ya
Ustawi wa Jamii, umeonesha kuwa jiji la Dar es salaam pekee lina watoto waishio
katika mazingira magumu elfu 5.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati
hiyo na Wakili wa kujitegemea Albert Msando, amesema kamati yake itajielekeza
katika kuangalia sheria na mapungufu yake kwa ajili ya kuzifanyia maboresho
Makonda aunda kamati maalum
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 18, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 18, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment