Lulu abadilishiwa adhabu, sasa kutumikia kifungo cha nje


Mcheza filamu, Elizabeth Michael maarufu Lulu amebadilishwa kifungo na sasa atatumikia adhabu hiyo akiwa nje yaani ‘kifungo cha nje’.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Novemba mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba

Akizungumza Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje amesema Lulu amebadilishiwa adhabu  na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam

“Lulu amebadilishiwa adhabu na ameachiwa juzi Jumamosi kati ya saa 2 hadi 3 asubuhi. Hii si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo chake nje, kitaalamu tunaita ‘community service’” amesema Mboje

Lulu abadilishiwa adhabu, sasa kutumikia kifungo cha nje Lulu abadilishiwa adhabu, sasa kutumikia kifungo cha nje Reviewed by KUSAGANEWS on May 14, 2018 Rating: 5

No comments: