Mbunge wa Arumeru Mashariki
(Chadema) Joshua Nassari amesema Serikali imewarudisha Watanzania katika
kipindi cha ukoloni ambako waliporwa ardhi yao bila sababu za msingi.
Nasari amesema kitendo cha kuwachomea
nyumba wananchi wa Meru kinawakumbusha miaka ya 1950, ambapo walilazimika
kuchanga fedha na kumtuma Japhet Kilila Nguro kwenda Umoja wa Mataifa kwa ajili
ya kutetea ardhi yao.
Akichangia katika hotuba ya Wizara
ya Maliasili na Utalii, jana Mei 21, mbunge huyo alizungumza kwa hisia kali
kuwa jambo kama hilo linawakumbusha mbali Watanzania na kuona kuwa bado wako
katika kipindi cha ukoloni walipokuwa wakiporwa ardhi bila hata kusikilizwa.
“Mimi sijui tunawasaidia akina nani
Tanzania yetu hii, wafanyabiashara wanalia, wavuvi wanalia, wananchi wanalia na
mnawapora ardhi hivi mnataka kutawala nani lakini?” Alihoji Nasari
Alisema mali walizoachiwa Watanzania
na Mungu zimeshindwa kuwa baraka tena na badala yake zimegeuka kuwa laana kwa
Watanzania na kuwafarakanisha.
“Mnatutonesha kidonda sisi watu wa
Meru, angalia picha hizi zinaonyesha haya ni maganda ya risasi na hizi ni picha
za mifugo ambayo imedhoofu sana iliyosababisha wananchi kubaki maskini kabisa,”
alisema Nasari
Joshua Nassari: Serikali Inawarudisha Watanzania Enzi za Ukoloni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 21, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 21, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment