Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limetoa onyo kwa wazazi na walezi wanaowafanyia watoto vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuwajeruhi ama kuwatelekeza na kuwafanya watoto hao kuishi katika mazingira hatarishi kuacha mara moja kwani wanachokifanya ni kosa kisheria.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoano Mwanza Ahmed Msangi ambapo amesema vipo vifungu vya sheria vinavyowapa mamlaka Jeshi la Polisi kuwakamata watu wanaowatendea ndivyo sivyo watoto kwa makusudi
Mbali na hilo, Kamanda Msangi amesema endapo itatokea mzazi atakaebisha kufanya hivyo kwa makusudi basi atakamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa mujibu wa sheria.
Jeshi la Polisi lawapa onyo wazazi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 21, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 21, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment