Kitaalamu
chakula unachokula leo ndio kinaamua hali ya afya yako kwa siku za usoni. Na ni
muhimu sana kuzingatia ulaji bora wa chakula na si kula ilimradi umekula.
Wataalamu wa lishe wanatuambia kuwa ulaji unaofaa hutokana na kula chakula
mchanganyiko kulingana na wakati
Lakini hata
ulaji huo, unatakiwa kutazamwa ni ulaji gani unaofaa kulingana na mchanganyiko
kulingana na mahitaji ya mwili. Na pia, wanasema mlo kamili unaofaa ni ule ulio
na virutubisho vyote muhimu kwa ajili ya lishe na afya bora.
Leo katika makala haya, yataangazia ulaji wa
tende, na kwa kuzingatia kuwa huu ni Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, tende ndiyo
tunda pekee linaloliwa kwa wingi, pengine kuliko tunda lingine lolote
Inaelezwa kuwa
kisayansi, tunda hilo limethibitika kusheheni madini na vitamini nyingi kiasi
cha kulifanya liwe na faida nyingi kiafya
Ulaji wa tende
kwa waliofunga
Mtaalamu wa
Lishe, Juliana Majaliwa anasema mtu aliyekwenye mfungo, mara zote huwa kiwango
chake cha sukari mwilini hupungua na kutakiwa airejeshe tena kwa kula vyakaula
vitakavyosaidia kufanya mara tu anapotakiwa kufuturu
Majaliwa
anasema aina ya kwanza ya sukari itumikayo mwilini ni ya glukosi. Lakini sukari
inayoshuka kwa watu ambao hawajala wala kula kwa muda mrefu, inaweza
kuwasababishia kupatwa na kizunguzungu au kulegea
Hivyo, anasema
ulaji wa tende mara mtu anapotakiwa kufuturu, humfanya aliyefunga asijihisi
kuchoka sana na huwa na nuru zaidi ya macho.
Pia tende
zitamsaidia kuimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji wa chakula tumboni, hivyo
ataondokana na matatizo ya ukosefu wa choo au matatizo ya kupata choo kigumu
kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia
Hivyo,
mfungaji akila tende zitamsaidia kupata virutubisho vya ‘amino acids’ ambavyo
ni muhimu mwilini, pia mwili wake utapata aina mbalimbali za madini na vitamin
za kutosha, ambazo zinapatikana kwenye tunda hili maarufu ambalo lina kiasi
kidogo cha mafuta yasiyo na lehemu.
Majaliwa
anasema sukari inapoliwa kwa njia ya chakula au kinywaji, mara zote viwango vya
glukosi ya mwili hujisawazisha yenyewe na kumfanya mlaji aliyefunga asijihisi
Ingawaje tende
mara nyingi si chakula kinachopendelewa sana na watu wenye njaa, lakini ndicho
chakula kisicho na mafuta na ni chanzo madhubuti cha sukari
Wataalamu wa
lishe wanasema mfungaji akila tende, atajipatia kiasi cha kutosha cha protini
na vitamin B1, B2, B3, B5, A1, na C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ustawi
wa afya ya mwili kwa ujumla
Faida zaidi za
tende
Wale walio
kwenye mfungo, muda wa kufuturu ukiwadia, wanashauriwa pia kuchanganya tende na
maziwa halisi kisha wale. Na kama wanajisikia uchovu, badala ya kunywa vinywaji
baridi vinavyodaiwa kuongeza nguvu, wale tende hata punje tatu tu zinatosha
Wataalamu wa
lishe wanawashauri kuanza kufungua kwa kula tende ili kuurejeshea mwili nguvu
iliyopotea kwa siku nzima
Kwa sababu
tende pia ina madini aina ya potasium na kiasi kidogo cha chumvi. Madini haya
husaidia uimarishaji wa mishipa ya fahamu. Watafiti wamegundua kwamba ulaji
kiasi wa madini ya potasium husaidia kumwepusha mtu na maradhi ya kiharusi. Pia
tende husaidia kupunguza lehemu mwilini
Wenye matatizo
ya kukauka damu
Wataalamu
wanasema kwa mfungaji mwenye tatizo la kukauka damu mwilini (anemia), anaweza
kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi ambayo ina kiwango cha kutosha cha
madini ya chuma ambayo huhitajika katika utengenezaji wa damu mwilini.
Wakati
vitu vingine vitamu vinadaiwa kuwa huozesha meno, lakini wataalamu wa tiba
lishe wanasema utamu wa tende huzuia uozaji wa meno
Faida zingine
za tende
Kwa mtu aliye na tatizo sugu la kukosa choo,
anatakiwa kuloweka tende za kutosha kwenye maji kiasi cha lita moja kwa muda
ili kupata juisi nzito, muathirika anywe na atapata choo laini.
Kwa matatizo
ya ukosefu wa nguvu za kiume, mchanganyiko maalum wa tende, maziwa, asali na
unga wa hiriki vinaweza kuondoa tatizo hilo. Chukua kiasi cha kiganja kimoja
cha tende, loweka kwenye maziwa ya mbuzi kiasi cha lita moja, ziache zilowane
kisha zisage kwenye maziwa hadi zichangayike, weka vijiko vitatu au vinne
vikubwavya asali pamoja na nusu kijiko cha chai cha hiriki, kisha kunywa mchangayiko
huo kila siku hadi utakapoona mabadiliko ya kuridhisha
Tende ni dawa
Tunaelezwa
kuwa tende ni dawa ya unene na kwa wale wenye matatizo ya wembamba wa
kupindukia na wanataka kuongeza uzito, ulaji wa tende kila siku unaweza
kuwasaidia. Lakini hii ina maana wale wanaohitaji kupunguza uzito, ulaji wa
tende kwa wingi hauwezi kuwafaa
Mtaalamu wa
tiba ya mimea, Japhet Lyatuu, anasema tende hutibu pia saratani ya tumbo na
husaidia pia kuondoa hali ya ulevi kwa wale wanaokunywa pombe
Anasema tende
tiba ni na haina madhara yoyote kwa sababu ni dawa ya asili na inafanyakazi
vizuri kuliko dawa za ‘kizungu’.
Laytuu anasema
tunda hilo husaidia pia kuimarisha nuru ya macho na tatizo la kutokuona usiku.
Anasema faida za tende ni nyingi na mtu anaweza kuila kwa namna mbalimbali.
Jinsi tende zinavyorejesha nguvu kwa waliofunga Ramadhan
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment