Serikali kupitisha umeme chini ya bahari

Serikali imesema itapitisha umeme chini ya bahari kutoka Nyamisati wilayani Rufiji mkoa wa Pwani hadi Kilindoni Wilaya ya Mafia na kubainisha kuwa kuna njia mbadala ya kuwapatia nishati hiyo kwa gharama nafuu wananchi wa maeneo hayo

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa Mei 25, 2018 bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ambaye alibainisha kuwa Serikali imeshakamilisha tafiti na kujiridhisha kuwa uwezekano wa kuvusha umeme huo upo

Amesema pia kuna uwezekano wa kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo mchanganyiko vya umeme wa jua, upepo na mafuta
Ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa Mafia (CCM), Mbaraka Baraka Dau aliyehoji ni lini Serikali itavusha umeme chini ya bahari kutoka Nyamisati kwenda Kilindini, eneo lenye umbali wa kilomita 50.

Serikali kupitisha umeme chini ya bahari Serikali kupitisha umeme chini ya bahari Reviewed by KUSAGANEWS on May 25, 2018 Rating: 5

No comments: