Wataalamu wa
afya duniani wamekuna vichwa na kupiga hatua. Wametoa mwanga wa matumaini kwa
wananchi wengi
Raia wa
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) huenda sasa wakaanza kupepesa macho na
kuvuta pumzi kwa furaha baada ya maofisa wa afya kuanza kutoa chanjo katika mji
wa Mbandaka uliokumbwa na visa vya ugonjwa wa ebola
Kuanza
kutolewa kwa chanjo hiyo ni matokeo ya juhudi za muda mrefu zilizowagonganisha
vichwa wataalamu kutoka kona mbalimbali duniani
Chanjo hiyo
ilidhibitika kuwa sasa ni madhubuti kuanza kutumika baada ya kufanyiwa ukaguzi
kwa muda wa miaka miwili kabla ya wataalamu hao kuja na kauli moja itumike.
Majaribio hayo yalipata nguvu zaidi mwaka 2014 wakati ugonjwa huo ulipozikumba
nchi kadhaa za Afrika Magharibi na kusababisha watu zaidi ya 11,000 kupoteza
maisha
Kufikia sasa,
watu 25 wamethibitishwa kufariki dunia tangu ugonjwa huo ulipozuka mwishoni mwa
Aprili huko Congo. Chanjo hiyo imekuwa ikitolewa kwa ushirikiano kati ya
Shirika la Afya Duniani (WHO) na Serikali ya Congo
WHO ilisema
makundi ya kwanza kupatiwa chanjo hiyo ni wahudumu na baadaye itasambazwa kwa
wananchi katika eneo ambalo virusi hivyo vimeripotiwa kuibuka
Ugonjwa wa
ebola unatajwa kuwa ni miongoni mwa magonjwa hatari duniani na mara nyingi
husababisha vifo vya ghafla. Ripoti zinasema idadi ya watu waliofariki dunia
kutokana na maradhi ya nchini Congo imeongezeka hadi watu 27
Wizara ya Afya
ya Congo imesema kumeripotiwa kifo kimoja zaidi katika eneo la Wangata mjini
Mbandaka ambako ndiko ulikozuka kwa mara ya kwanza mwaka huu. Kufikia sasa kuna
visa 51 vya ebola vilivyoripotiwa nchini humo tangu mlipuko huo ulioripotiwa
kwa mara ya kwanza na kati ya visa hivyo 28 vimethibitishwa
Kuzuka kwa
ebola kunasababisha kujaribiwa kwa chanjo mpya ya ugonjwa huo ambayo ilionekana
kufanya kazi vyema Afrika Magharibi miaka michache iliyopita. Zaidi ya vipimo
4,000 vya chanjo hiyo vimewasili nchini Congo wiki hii huku vipimo zaidi
vikitarajiwa kufika
Changamoto kuu
itakuwa kuiweka chanjo hiyo katika hali ya baridi katika eneo ambalo lina
miundo mbinu duni na umeme katika sehemu chache
Tangu mwaka
1976, huu ni mlipuko wa tisa wa ebola nchini Congo hali ambayo imewafanya
wataalamu waanze kuna vichwa vyao mara mbilimbili
Virusi vya
ugonjwa huu vinasambazwa kwa watu kutoka kwa wanyama wa porini wakiwemo popo na
tumbili. Hadi sasa wakati wataalamu wakiendelea kutoa chanjo hakuna tiba maalum
ya ugonjwa huo
Dalili zake ni
homa, kutapika, kuharisha, maumivu ya misuli na wakati mwingine kuvuja damu
ndani na nje ya mwili. Ebola inaweza kusababisha vifo katika asilimia 90 ya
visa
Duru za habari
zinasema chanjo hiyo inatarajia kupanuliwa zaidi kuanzia leo huku watu 600
wakilengwa kupatiwa. Hata hivyo, shirikisho la msalaba mwekundu limeonya kuwa
bado mlipuko huo haujadhibitiwa kikamilifu na kusisitizia jamii kuwa waangalifu
na kuwazika watu waliokufa na ugonjwa huo kwa njia salama ili kuepuka
maambukizi zaidi.
Ugonjwa umesambaa kutoka maeneo ya mashambani
hadi katika mji wa Mbandaka, ambao ni kitovu muhimu cha shughuli za uchukuzi
katika maeneo yanayounganisha Mto Congo. Jambo hilo linadaiwa kuongeza wasiwasi
kwamba huenda maradhi hayo yakasambaa hadi katika mji mkuu Kinshasa au nchi
jirani
Hata hivyo,
shirika hilo limeeleza imani yake kwamba ugonjwa huo utadhibitiwa.“Tuna imani
kwamba hali hii itakabiliwa ili kutoleta madhara zaidi,” lilisema kwenye
taarifa
Juzi, Naibu
Waziri, Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile
alisema hadi sasa Tanzania bado haijakumbwa na virusi vya ugonjwa huo na
akaahidi kuendelea kuongeza udhibiti katika maeneo ya mipakani.
Tangu wiki iliyopita mikoa ambayo imepakana na
Congo, ikiwemo Kigoma, Katavi na Rukwa wananchi wanaingia nchini kupitia maeneo
hayo yamekuwa wakifanyiwa uchunguzi ili kubaini kama wameambukizwa maradhi hayo
Katika mkutano
wa dharura uliofanyika baada ya kuzuka kwa ugonjwa huo wataalamu wa WHO
walisema hali ebola nchini Congo haijafikia ya kuutangaza “janga la kimataifa”.
Tayari, kamati
yake ya huduma za dharura imetoa ushauri maalum kwa serikali ya taifa hilo
kuendelea kushirikiana ili kuimarisha mikakati ya kukabili maenezi ya ugonjwa
huo. “Bila ushirikiano wa kutosha, kuna hatari kwamba hali hii itakuwa mbaya
zaidi,” ilionya kamati ya wataalamu wa WHO kupitia taarifa yake iliyotolewa
baada ya mkutano wa dharura
Aidha, kamati
pia imetoa wito kwa jamii ya kimataifa, wanasayansi na wataalamu wa afya
kushirikiana ili kutoa habari muhimu zitakazosaidia kupatikana kwa tiba yake.
Wataalamu wa WHO wamesema hatua za haraka
zimeweza kuzuia kuenea kwa mlipuko huu mpya uliotangazwa siku 12 zilizopita
Chimbuko la
virusi vya ebola
Virusi vya
ebola ni vidogo kiasi kwamba ni vigumu kuweza kuonekana kwa macho ya kawaida.
Vinaweza kuonekana kwa njia ya darubini vikionekana kama uzi pindi
vinapochunguzwa na chombo hicho
Virusi hivyo
viligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1976 na watafiti wa magonjwa katika
kijiji kimoja katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (zamani ikiitwa Zaire
Virusi hivyo
vilipewa jina la ebola kuashiria jina la mto unaopakana na kijiji hicho, ambao
ni Mto Ebola. Baadaye kulizuka milipuko mingine mitatu nchini humo na pia chini
Sudan katika miaka ya 1970.
Baadaye virusi hivyo vilipotea hadi mwaka 1994
wakati ugonjwa huo ulipozuka tena. Kuzuka kwa ugonjwa wa ebola nchini Gabon,
ndio ulikuwa mwanzo wa kusambaa kwa virusi hivyo hadi katika mataifa mengine ya
Afrika Magharibi
Hadi sasa
ugonjwa huu wa ebola umezuka mara 20 ingawa mara nyingi umekuwa ukidhibitiwa.
Wakati wote huo ugonjwa huu ulipozuka, idadi ya watu walioambukizwa haikuwa
kuzidi 430
Mara ya mwisho
ebola ilizuka nchini Guinea mwaka 2013 na kisha kwa haraka ulisambaa hadi
nchini Sierra Leone na Liberia ambako watu 11,000 walifariki dunia na wengine
zaidi ya 10,000 kuambukizwa virusi hivyo.
Ugonjwa huu sasa umetangazwa kuwa
janga katika mataifa hayo
Mojawapo ya
sababu zinazotajwa kuchangia kusambaa kwa virusi vya ugonjwa huu wa ebola, ni
kwamba mwanzoni mataifa yaliyoathirika na hata jamii ya kimataifa ilipuuza
uzito wa janga hili
Tangu kuzuka
kwa ugonjwa huo katika mataifa ya Afrika Magharibi, juhudi za kupata dawa ya
kuutibu zimeimarishwa kote duniani.
Shirika la
Afya Duniani (WHO) lina matumaini ya kutoa chanjo kwa maelfu ya watu wanaoishi
katika mataifa yanayoathirika zaidi na ugonjwa huu kufikia katikati ya mwaka
2019.
Hata hivyo hilo halikufanikiwa mpaka chanjo hiyo ilipobidi kusubiri kwa
muda wa miaka kadhaa ikiendelea kufanyiwa majaribu
Awali WHO
ilikadiria kuwa kufikia mwishoni mwa mwaka huo wa 2015 lingekuwa limetoa chanjo
kwa watu milioni moja dhidi ya ugonjwa huo
Kuanza
kutolewa kwa chanjo hiyo nchini Congo kumeleta matumaini siyo tu kwa taifa hilo
bali hata kwa mataifa jirani yaliyoanza kujihami na maambukizi yake.
Mwanga wa matumaini chanjo ya ebola huu hapa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment