Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika mwaka wa fedha 2018/19 imeongezeka
kutoka Sh 1.72 trilioni ya mwaka wa fedha 2017/18 na kufikia Sh 1.91
trilioni
Kati ya fedha hizo Sh 1.67
trilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh 234 bilioni ni kwa ajili
ya kugharamia shughuli za maendeleo
Akiwasilisha bajeti hiyo bungeni
leo Mei 14, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi
amesema wizara katika utekelezaji wa bajeti yake ya mwaka 2017/18
imekabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni upungufu wa rasilimali fedha
Amesema kiwango
kilichoidhinishwa na bunge kilikuwa Sh 1.72 trilioni katika bajeti ya mwaka
wa fedha 2017/18 ni kidogo ikilinganishwa na mahitaji halisi ya Sh 3.2
trilioni
Aidha, amesema bajeti
iliyoidhinishwa kwa upande wa fedha za maendeleo hutolewa kwa kiwango
kidogo
“Hali hii imesababisha
kulegalega kwa utoaji wa huduma na wizara kuendelea kuwa na madeni yanayoathiri
utendaji wa wizara na kupoteza uaminifu kwa wazabuni wanaotoa huduma na
kuleta bidhaa mbalimbali,” amesema
Dk Mwinyi amesema hadi kufikia
Aprili mwaka huu, wizara ilikuwa imepokea Sh 181.58bilioni sawa na asilimia
82.91 bilioni kati ya Sh 219 bilioni zilizoidhinishwa na bunge katika
bajeti ya 2017/18 kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo
|
No comments:
Post a Comment