Afisa Uhamiaji mkoa wa
DSM,Chrispine Ngonyani amebainisha raia kutoka nchi ya Ethiopia wamekuwa
wakiwasumbua idara ya uhamiaji nchini kwani kila mara wanapokamatwa wahamiaji
haramu wao huwa ni wengi zaidi.
Bw. Ngonyani amezungumza hayo wakati
akitoa taarifa za utendaji kazi wa idara hiyo kwa wanahabari ambapo amesema
kuwa tatizo la raia kutoka Ethiopia siyo tu kwa uhamiaji Dar es salaam
bali nchi nzima wanakumbana nalo.
"Raia wa Ethiopia
wanatusumbua sana yaani kila tukikamata watuhumiwa kwa wingi, basi unakuta ni
waethiopia ambao hawapungui 50 hadi 80 hilo ndo kundi la watu wanaotusumbua
sana Idara ya Uhamiaji mkoa wa Dar es salaam" amesema.
Pamoja na hayo Bw. Ngonyani ameeleza
kuwa idara hiyo kwa kipindi cha mwezi Januari 2018 hadi Mei 24, 2018
wameafanikiwa na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa 602 ambapo kari yao
watuhumiwa 227 walikuwa raia wa Ethiopia na kati ya mashauri 118
yaliyofunguliwa Mahakama ya Kisutu raia wa Ethiopia walikuwa 214 na kati ya
mashauri yaliyomalizika yalikua 99 na kati ya watuhumiwa 341 raia wa Ethiopia
walikuwa 218.
Mbali na hayo Afisa huyo amesema
Idara imefanikiwa kuingiza faini ya shilingi Milioni 121.5 na kati watuhumiwa
waliofungwa ni 187 na mashauri yanayoendelea mahakamani ni 73 huku raia 28
wakupewa oda ya kurudishwa kwao.
aethiopia waitesa uhamiaji Tanzania
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment