Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amefunguka na
kumpongeza Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe
kwa kuendelea kumpigania diwani wa CCM Simon Kanguye ambaye amepotea kwa
kutekwa toka mwaka jana.
Zitto Kabwe alihoji bungeni juu ya
kupotea kwa Simon Kanguye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri Kibondo
ambaye anadaiwa kutekwa miezi 9 sasa na hafahamiki wapi yupo hivyo alihitaji
vyombo vya usalama viweze kuweka wazi jambo hilo ili wajue kama ameshakufa ili
waweke matanga au kama wao wanamshikilia.
Kufuatia taarifa hiyo serikali
kupitia kwa Waziri Mkuchika ndipo ikaweka wazi kuwa jambo hilo lipo chini ya
jeshi la polisi lakini alitumia nafasi hiyo kumpongeza Zitto Kabwe kwa kuweza
kufuatilia jambo hilo ili hali diwani huyo ni mwanachana wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM).
"Navyomuelewa Zitto Kabwe
alivyo msomi, kijana anayeipenda nchi yake tena ana akili simuoni Zitto
anahamasisha watu kuchukua sheria mkononi bali yale maneno aliyaweka tu
kutuhimiza watu wa serikali jamanii eehh fanyieni kazi, na sisi tumelipokea,
ila suala la kupotea kwa diwani huyo lilisharipotiwa polisi na uchunguzi
unaendelea na tena hapa nampongeza ndugu yangu Zitto Kabwe huyu diwani
anayemtetea tumtafute mpaka tumpate wala siyo wa chama chake cha ACT Wazalendo
bali ni diwani wa CCM hii inaonyesha jinsi alivyomzalendo, anavyopenda haki
itendeke kwa kila mtu sasa uendelee hivyo hivyo mdogo wangu Zitto usiyumbe
kwenye mengine endelea hivyo hivyo" alisisitiza Mkuchika
Zitto Kabwe endelea hivyo hivyo - Mkuchika
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment