Mvua zinazoendelea
kunyesha sehemu mbali mbali nchini zimeendelea kuleta madhara mkoani Rukwa,
ambako zimeteketeza mashamba ya vyakula na kuharibu kabisa mazao.
Akizungumza na Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa,
George Kyando amesema mvua hizo zimezoa kabisa mazao kwenye mashamba mkoani
humo na mengine kuyafunika kwa udongo, hali ambayo imeleta hasara kwa wakulima.
Sambamba na hilo Kamanda Kyando
amesema pia barabara mbali mbali zimekatika na kukosa mawasiliano kabisa, huku
baadhi ya madaraja yakizolewa na maji, lakini hakuna tarifa ya vifo waliyoipata
mpaka sasa.
“Huku Rukwa kuna barabara inayopita
bonde kwa bonde kutoka mkoa wa Rukwa kwenda Katavi, kutokana na hizi mvua
zinazonyesha madaraja yamechukuliwa na maji, bara bara imekatika, mashamba ya
mipunga na mahindi yamefunikwa na udongo, kwa hiyo tumepata hayo majanga lakini
tunashukuru Mungu hakuna mtu yeyote ambaye amedhurika na hiyo mvua, ni miundo
mbinu na mashamba tu”, amesema Kamanda Kyando.
Kutokana na mvua hizo Mamlaka ya
hali ya hewa Tanzania imewataka wananchi kuwa makini wanaposafiri na kutembea,
kwani mvua kubwa zaidi inatarajiwa kunyesha siku za hivi karibuni.
Mvua zaharibu mazao Rukwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment