Mjukuu wa Malkia
Elizabeth wa Uingereza, William Arthur amemuahidi Makamu wa Rais Samia Suluhu
kuwa ataisaidia Tanzania katika kuboresha ulinzi wa wanyama pori kwa kutumia
teknolojia ya hali juu na kumualika Rais Magufuli katika mkutano wa masuala ya
wanyapori utakaofanyika Oktoba 2018.
Prince William ameeleza hayo wakati
alipokutana na kufanya mazungumzo na Mama Samia leo katika Jumba la Kifalme la
Buckingham Palace nchini Uingereza ambapo Makamu wa Rais amekwenda kumuwakilisha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano
wa wakuu wa nchi na serikali wa nchi za jumuiya ya Madola.
Kwa upande wake Makamu wa Rais
alimweleza Prince William kuwa Tanzania inatambua mchango wake katika kuzuia
ujangili wa wanyama pori na serikali ya Tanzania imekuwa ikichukua hatua
mbalimbali ya kupambana na kuzuia ujangili ingawa bado haijawa na teknolojia
yenye uwezo wa wa kutambua na kuona wanyama wote lakini wameendelea kuimarisha
ulinzi wa wanyama pori.
Mtazame hapa chini Makamu wa Rais
Samia Suluhu akiwa anazungumza na Prince William
Prince Wiliam kuipa Tanzania ulinzi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment