Zaidi ya watoto elfu ishirini wenye umri wa miaka 14
kutoka wilaya zote saba za Mkoa wa Arusha wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya
saratani ya shingo ya kizazi ili kuwakinga na ugonjwa huo
Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Arusha Aziz Sheshe amesema
chanjo hiyo itaanza kutolewa rasmi tarehe 25 mwezi huu katika vituo vya afya
292 na katika shule zitakazo ainishwa ikiwa ni pamoja na vituo maalum
vitakavyokuwa katika ofisi za vijiji.
Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema ni vema jamii ikaondokana na mila
potofu na upotoshaji
utakaokwamisha zoezi hilo kwani chanjo hiyo ni salama na itaokoa maisha ya watoto wa kike; kwa kuwa
hadi sasa asilimia 50 ya vifo vyote vinatokana na saratani ya shingo ya kizazi
na matiti.
Naye mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Timothy Onanji
ameeleza kuwa chanjo hiyo ni juhudi za
serikali ili kuleta maendeleo katika kupambana na ugonjwa huo unaokua kwa kasi.
Aidha Naibu meya wa Jiji la Arusha Viola Lazaro akiongea
kwa niaba ya wanawake amesema chanjo
hiyo ni mkombozi kwa wanawake katika
taifa kutokana na matibabu ya ugonjwa huo kuwa na garama kubwa hivyo wajitokeze
kwenda kupata chanjo hiyo kwani afya njema inajenga taifa bora.
ZAIDI YA WTOTO 20,000 ARUSHA KUPATIWA CHANJO YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment