Mbunge wa Kigoma (ACT-Wazalendo), Zitto
Kabwe amesema kitendo cha mawaziri kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG), ni kinyume cha Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma na
kifungu 38 (1 na 2).
Akizungumza leo Aprili 15 mjini hapa, Zitto amesema kifungu hicho kinaeleza namna hoja hizo zinavyotakiwa kujibiwa na kwamba mawaziri wamekuwa hawatajwi kabisa katika kifungu hicho
“Wanaopaswa kujibu hoja za CAG ni maofisa
masuhuli ambao ni makatibu wakuu wa wizara, siyo kujibu kwa kuita mikutano na
wanahabari bali kujibu kwa kutokea katika kamati (za Bunge za Hesabu),” amesema.
Amesema kinachofanwa na mawaziri ni kinyume
cha sheria na kwamba, sheria imeweka adhabu kwa makosa hayo ya juu
kabisa ikiwa ni kifungo cha miaka miwili jela au faini ya Sh5 milioni
“Nawasihi mwenyekiti wa kamati ya PAC na
mwenyekiti wa kamati ya LAAC wafikishe jambo hili kwa Spika ili
amuandikie Waziri Mkuu kumweleza kuwa, mawaziri wanavunja sheria.
Kinachonisikitisha ni kuwa baadhi ya mawaziri waandamizi ndiyo wanaongoza zoezi
hili,” amesema.
Zitto awashukia mawaziri
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment