Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
amempongeza Rais mpya wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume
huku akisema chama hicho kitampa ushirikiano wa kutosha
Taarifa kwa umma iliyotolewa leo Aprili 15,
2018 na Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni
amewapongeza viongozi wengine waliochaguliwa sambamba na Fatma akisema,
“kukuchagua kuwa rais wa chama chao katika kipindi ambacho Taifa linamhitaji
mtu jasiri, makini na shupavu kama wewe
“Ushindi wako umetuma ujumbe kuwa mawakili
wa Tanganyika wanajua msimamo wako na wanaamini kwa dhati kuwa kwa kushirikiana
na viongozi wenzako mliochaguliwa kuongoza TLS utawavusha katika kipindi hiki
ambacho Taifa linapitia na kushuhudia majaribu mengi ya uvunjifu wa Katiba,
sheria na kanuni mbalimbali.”
Mbowe amesema, “umepokea kijiti katika
wakati ambao mtangulizi wako (Tundu Lissu) yuko hospitalini baada ya jaribio la
shambulizi lililolenga kumuua kushindikana.”
huyo ameendelea kusema, “tukutie moyo kuwa
Chadema kama taasisi ya kisiasa tukiwa wadau wa masuala ya haki, sheria na
utawala bora tuko nawe na tutaendelea kukupa ushirikiano wakati wote wa uongozi
wako, wewe na wenzako wote.”
Amesema wanampongeza kwa kuweka historia
ndani ya Taifa kwa kuwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo mkubwa kuongoza
TLS
Fatma alichaguliwa jana kuwa rais wa TLS katika mkutano mkuu wa mawakili uliofanyika mjini Arusha akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Lissu.
Mbowe ampongeza Fatma Karume
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment