Kesi ya jinai inayowabili vigogo wa Chadema
akiwamo mwenyekiti Freeman Mbowe kesho inaanza kuunguruma katika hatua ya
usikilizwaji wa awali, upande wa mashtaka utatoa picha kamili
Mbali na mbowe wengine ni Katibu Mkuu, Dk
Vicent Mashinji na manaibu katibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum
Mwalimu (Zanzibar
Wengine ni mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji
Peter Msigwa; Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha),
Esther Matiko na Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee pamoja na Mbunge wa Tarime
Vijijini, John Heche.
Washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na
jumla ya mashtaka 12 ya mikusanyiko na maandamano yasiyo halali na ya uchochezi
wa uasi, wakidaiwa kutenda makosa hayo Februari 16, 2018 wakati wa maandamano
yaliyosabasha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwilina
Akwiline
Wakati kesho vigogo hao wa Chadema
watakapopandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuna mambo
makubwa mawili yanayotarajiwa kuyojiri katika kesi hiyo.
Jambo la kwanza linalotarajiwa kutokea kabla
ya mambo yote ni kuunganishwa nao kwa mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya
Bulaya ambaye ni mmoja wa washtakiwa katika
kesi hiyo, alikuwa bado hajakamatwa na kuhojiwa kabla ya kupandishwa kizimbani
kama ilivyokuwa kwa wenzake, lakini April 13, aliitwa Kituo Kikuu cha Polisi na
kuhojiwa kabla ya kuachiwa kwa dhamana
Baadaye Katibu Mkuu wa Chadema, Mashinji
alilieleza Mwananchi kuwa mbunge huyo ataunganishwa nao katika kesi yao kesho
Hivyo, ikiwa kesho atafikishwa mahakamani,
basi ataunganishwa na wenzake katika kesi hiyo na katika kufanya hivyo upande
wa mashtaka ulazimika kubadili hati ya mashtaka ili kuwasilisha hati ya
mashtaka yenye majina ya washtakiwa wote akiwemo Bulaya
Jambo la pili litakalojiri kesho ni
usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo. Katika hatua hii upande wa mashtaka
utawasomea washtakiwa mashtaka yanayaowakabili na washtakiwa watatakiwa ama
kuyakana au kukubali mashtaka hayo
Ikiwa watayakubali, basi mahakama itawatia
hatiani na kisha kuwapa adhabu kwa mujibu wa sheria
Ikiwa watayakana mashtaka hayo, basi upande
wa mashtaka utawasomea muhtasari wa maelezo ya kesi. Huu ni muhtasari wa
ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka, kulinganma na upelelezi
Kisha washtakiwa baada ya kusomewa maelezo
hayo watatakiwa wabainishe mambo wanayokubaliana nayo, yaani mambo
yasiyobishaniwa na yale wasiyokubaliana nayo, yaani mambo yanayobishaniwa,
ambayo ndio upande wa mashtaka utapaswa kuyatolea ushahidi mahakamani
Pia, pande zote yaani upande wa mashtaka na
upande wa utetezi utapaswa kueleza idadi ya mashahidi pamoja na vielelezo
vitakavyotumika katika kesi hiyo, ingawa idadi ya mashahidi inaweza kupungua
kadri itakavyoonekana inafaa
Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo
Februari 16, 2018 katika Viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni na katika
Barabara ya Kawawa, Mkwajuni, Kinondoni
Mbowe kwa upande wake anakabiliwa na
mashtaka mengine matano zaidi yeye peke yake, huku Msigwa naye akikabiliwa na
shtaka moja zaidi peke yake.
Mambo mawili yatakayojiiri kesi ya akina Mbowe kesho
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment