Nchi ya Zimbabwe
imehalalisha uzalishaji wa bagi kwa matumizi ya kiafya na kisayansi.
Zimbabwe itakuwa nchi pili
kufanya hivyo barani Afrika baada ya Lesotho, ambayo ilitoa leseni yake ya
kwanza kwa kilimo cha mmea huo mwaka uliopita.
Waziri wa afya David Parirenyatwa
amechapisha sheria zinazowaruhusu watu na kampuni kupewa leseni ya kufanya kilimo
cha bangi ambayo hufahamika nchini humo kama mbanje, na kwamba watu wa nchi
hiyo sasa wanaweza kutuma maombi ya kulima bangi, na leseni yake itakuwa
inaombwa upya kila baada ya miaka mitano, na itawaruhusu wakulima kumiliki,
kusafirisha na kuuza bangi.
Watuma maombi watatakiwa kueleza ni
wapi watafanyia kilimo chao, kiwango ambacho wataweza kuzalisha na kuuza na
wakati wa kuzalisha bangi hiyo.
Nchini Zimbabwe ilikuwa ni haramu
kupanda, kumiliki au kutumia mmea huo nchini Humo, na iwapo mtu atapatikana na
makosa hayo anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 12 jela.
Zimbabwe yaruhusu bangi rasmi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 29, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 29, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment