Msanii wa filamu nchini
Tanzania na mwanasiasa Steve Nyerere amefunguka na kuwataka wasanii wenzake na
watu mbalimbali wasiende hospitali kumuona Mzee Majuto kwa lengo la kupigana
nae picha ili atakapo kuwa amefariki waweze ku-post aliyopiga nae bali waende
kumuona kwa ajili ya kuombea dua
Steve ametoa kauli hiyo wakati
akizungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuonekana wasanii na
watu maarufu mbalimbali wakionekana kuweka picha mitandaoni pindi walipokuwa
wamekwenda kumtembelea Mzee Majuto katika hospitali ya Tumaini Jijini Dar es
Salaam ambapo amelazwa mwanzoni mwa wiki hii kutoka na maradhi yake ya tezi
dume yanayomuandama.
"Twendeni tukamuone Mzee
Majuto, tusiende kumuona Majuto kwa ajili ya kupigana nae picha kwa sababu
wengi akili zao zinawaza kuwa atatutoka 'atafariki' mambo hayo ni ya Mwenyezi
Mungu. Wengi wanahofu kwamba akishafariki aweze kuwa na picha aliyokwenda
kumuona, naomba tufute hayo mawazo",
amesema Steve Nyerere
Pamoja na hayo, Steve ameendelea kwa
kusema "hakuna mtu yeyote duniani aliyesema kwamba kuumwa ni
kifo bali kuumwa ni ibada tu, inakukumbusha kuna Mungu. Kwa maana hiyo tusiende
hospitali kwa lengo la kupiga picha, twendeni hospitali kwa ajili ya maombi
yatakayomfanya mwenzetu asimame na michango kuhakikisha Majuto
anachangiwa".
Steven Nyerere akataa kupiga picha na Majuto
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 29, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 29, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment