Mbunge wa Mikumi kupitia
CHADEMA ambaye pia ni msanii mkongwe wa hip hop Bongo, Joseph Haule maarufu kwa
jina la Profesa Jay, amesema kwamba kitendo cha baadhi ya viongozi kuita
wasanii na kupiga nao picha bada ya kuwasaidia matatizo yao si sahihi, kwani
wasanii hao wana matatizo makubwa
Akizungumza Bungeni Prof Jay amesema
serikali haiwezi kuwa inachukua kodi kwa wasanii bila kuwatengenezea mazingira
mazuri ya kazi zao na kutatua changamoto zao, na kuitaka kuweka bajeti maalum
kwa ajili yao ili kutatua matatizo yao na sio kuishia kupiga nao picha.
“Huwezi ukamkamua ng'ombe kabla
hujamlisha majani, niwaambie serikali wekeni bajeti kwa wasanii, wana matatizo
makubwa kuliko hayo mnayodhani, maana mnadhani kuwasaidia wasanii wa Tanzania
ni kuwaalika sehemu za maofisini kwenu na kupiga nao picha, kupiga selfie na
vitu vingine, wasanii wa Tanzania wana matatizo makubwa, hawahitaji kula
ubwabwa na nyinyi, wanahitaji muwasaidie masuala ya kazi zao zinazoibiwa,
wanahitaji wasaidiwe wasuala ya masoko, wanahitaji wasadiwe mitaji”, amesema
Prof. Jay
Sambamba na hilo Prof. Jay ameitaka
BASATA kuwajibika kwenye kuwaelimisha wasanii kama ilivyopewa mamlaka yake, na
sio kuwa sehemu ya kutoa hukumu tu pale wanapokosea.
Prof. Jay awachana wanaopiga picha na wasanii
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 29, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 29, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment