Baba mdogo wa marehemu
Chacha Heche Suguta ambaye pia ni mdogo wa Mbunge John Heche, Bwana Issa
Suguta, amevitaka vyombo vya dola kulinda wananchi wake kama inavyopaswa, na
kama wameshindwa basi iwaache wananchi wajilinde wenyewe kwa namna wanayoijua.
Akizungumza na waandishi wa habari
waliofika kituo cha polisi mara baada ya wananchi kukizingira kufuatia
tukio hilo, Mzee Suguta amesema kwamba kama serikali imeshindwa kuwalinda
wananchi wake, basi iwape uhuru wa kujilinda wenyewe.
Mzee Suguta ameendelea kwa kuitaka
serikali ya awamu ya tano kuwatetea wanyonge pale inapobidi, kama ambavyo
inajitangaza kuwa ni serikali ya wanyonge.
“Tunaomba vyombo vya dola
vituangalie vitulinde, na kama hakuna ulinzi tujilinde wenyewe, kama mtu
anakuja kuuawa hapa, maaskari wanakamata mtu badala wapite naye kwenye lami,
wanapita naye nyuma kuja kumuulia sehemu kama hii, wananchi tuwaelewe vipi?
ninaomba serikali ya Magufuli kama kweli ni serikali ya wanyonge, muwatetee
wanyonge kama hawa waliopata shida hapa”, amesema Mzee Suguta.
Ijumaa ya April 27,
2018, Kijana Chacha Heche Suguta aliuawa kwa kuchomwa kisu na polisi wa
kituo cha Sirari Tarime, tukio ambalo limethibitishwa na Kamanda wa Mkoa wa
Kipolisi Tarime/Rorya Henry Mwaibambe, na kumshikilia polisi huyo aliyefanya
mauaji.
Baba wa Suguta Chacha afunguka
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 29, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 29, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment