Rais Dkt. John Magufuli
amewapongeza wananchi wa Mkoa wa Iringa kwa kuweza kupata barabara ya uhakika
na kuwataka kuongeza juhudi katika uzalishaji mali hasa katika kilimo na
biashara ili waweze kunufaika nayo nasio vinginevyo.
Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo leo
Aprili 29, 2018 wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza katika ufunguzi wa
barabara ya lami ya kutoka mkoani Iringa kuelekea Migoli hadi Fufu yenye urefu
wa kilomita 189 na ambayo inaunganisha Mkoa wa Iringa na Mkoa wa Dodoma.
Aidha, Dkt. Magufuli amesema pamoja
na kujenga barabara hiyo, serikali inauboresha uwanja wa ndege wa Nduli ili
uweze kupokea ndege kubwa zitakazoweza kupokea watalii wengi na wafanyabiashara
katika mkoa wa Iringa na maeneo mengine ya kusini mwa Tanzania ili rasilimali
zilizopo katika maeneo hayo ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ziwanufaishe
wananchi kama wanavyonufaika wananchi wa Kaskazini mwa Tanzania.
"Ruaha ni hifadhi kubwa, nataka
hifadhi hii iwe kitovu cha utalii, nataka nyinyi ndugu zangu wa Iringa mnufaike
na utalii katika hifadhi hii kama wanavyonufaika kule kaskazini kupitia
Serengeti, watalii wakija hapa wenye hoteli watapata wateja, wenye maziwa
watauza, wenye matunda watauza, wenye mahindi watauza, mtapata
hela", amesema Rais Magufuli.
Kwa upande mwingine, Rais Magufuli
amewataka wananchi wa Iringa kuwapuuza wanaodai Serikali inakopa sana, na
kueleza kuwa fedha hizo hukopwa kwa masharti nafuu, riba ndogo na hulipwa kwa
muda mrefu, na kwamba ndizo zinatumika kujenga miundombinu ya kuchochea uchumi.
Rais Magufuli aweka wazi lengo la serikali yake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 29, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 29, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment