Klabu ya soka ya Simba
imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga kwenye pambano la watani wa Jadi,
lililopigwa kwenye uwanja wa taifa jioni hii na kujiweka kwenye mazingira
mazuri ya kutwaa ubingwa.
Simba ambayo imeongoza ligi kwa muda
mrefu leo iliingia uwanjani ikipewa nafasi kubwa ya kushinda na pengine kwa
mabao mengi zaidi, lakini bao pekee la mlinzi mkongwe Erasto Nyoni dakika 37
limeamua mchezo.
Mazingira ya mabao hilo yalianzia
kwa Kevin Yondani kumchezea rafu Shomari Kapombe na kusababisha adhabu ndogo
ambapo mpira huo ulipigwa na Shiza Kichuya na kutua kichwani kwa Nyoni ambaye
aliutumbukiza nyavuni.
Baada ya ushindi huo Simba sasa
imefikisha alama 62 kwenye mechi 26 huku ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja
kwenye ligi kuu msimu huu. Sasa Simba inabakiza alama 4 pekee ili iweze
kuwa bingwa msimu huu.
Kwa upande mwingine kwenye mchezo wa
leo Yanga walilazimika kucheza pungufu kwa takribani kipindi chote cha pili
baada ya beki wa kulia Hassan Kessy kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 49
kutokana na rafu aliyomchezea Asante Kwasi.
Simba waimaliza Yanga, waunusa ubingwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 29, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 29, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment