Wiki ijayo zamu ya wababa - Paul Makonda


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefunguka na kusema kuwa familia 170 ambazo zilikwenda jana ofisini kwake waliweza kuelewana namna ya kulea watoto wao na kusema zoezi linakwenda vizuri kama ambavyo lilikusudiwa na kudai kuanzia Jumatatu sasa wataanza kuitwa wakina baba.  

Makonda amesema hayo April 12, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari na kutolea ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali ikiwepo watu ambao wamesema ni watoto wa viongozi fulani na hawajafika ofisini kwake amewasihi kufika ofisi kwa kuwa wao wanafanya kazi na watu ambao wamekwenda ofisini na si wale ambao wanajirekodi kwenye mitandao ya jamii. 

"Hatimaye tunaona familia zinarudi katika msingi wake zoezi hili tunaendelea nalo leo na kesho tutaona idadi tutakayoifikia kwani lengo tukishamalizana na kina mama Jumatatu tutawaita wakina baba ambao wengine wameshaanza kuja na wengine tutawaita kwani lengo la serikali ni kuhakikisha ustawi unaanzia kwenye familia" alisema Makonda 

Aidha Makonda amesema kuwa watoto ambao wametelekezwa na baba zao labda wapo nje ya Tanzania au wamefariki basi watajitahidi kuhakikisha wanampunguzia machungu mama wa mtoto kwa kuwaandikishia bima ya afya na kudai kuna mtu amejitolea zaidi milioni 250 kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya watoto hao. 

Wiki ijayo zamu ya wababa - Paul Makonda Wiki ijayo zamu ya wababa - Paul Makonda Reviewed by KUSAGANEWS on April 12, 2018 Rating: 5

No comments: