Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akizungumza na wanahabari kwenye Ukumbi
wa Bunge, mapema leo ktolea ufafanuzi hoja zilizobainishwa kwenye Ripoti ya
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Waziri
wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo
amesema katika Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali,
Halmashauri zilizopata Hati Safi zimeongezeka kutoka
Halmashauri 81 kwa mwaka 2015/16 mpaka kufikia Halmashauri 166 (90%) kwa
mwaka 2016/17.
Jafo ameyasema hayo wakati kwa Kikao na
Waandishi wa Habari kilichofanyika katika ukumbi Bunge kuhusu utekelezaji wa
baadhi ya mapendekezo ya CAG kwa hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa
mwaka Ulioishia Juni 30, 2017.
Alisema “napenda kutoa shukrani zangu za
dhati kwa Wenyeviti na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali za Mitaa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa
kwa maelekezo yao mazuri yaliyosaidia sana utendaji kazi wa Ofisi ya Rais –
TAMISEMI, Mikoa na MSM; Michango yao, ushauri na maelekezo yamewezesha kuongeza
Idadi ya Hati Safi.
Akizungumzia kuhusu hoja zilizobainishwa
katika ropoti ya CAG Mhe. Jafo alisema tumefanyia kazi mapendekezo yote
yaliyotolewa katika ripoti zilizopita ambapo watumishi 434 wamechukuliwa hatua
baada ya kubainika kusababishia halmashauri zao hasara/hoja zisizo za lazima
kutokana na kutotekeleza ipasavyo wajibu wao ama kujihusisha na vitendo vya
ubadhirifu.
“Kati ya hao 9 wamefukuzwa kazi, Watumishi
210 wamepewa barua za onyo huku Watumishi 15 wakifikishwa kwenye vyombo vya
dola. Watumishi 28 wamesimamishwa kazi, 13 wametakiwa kufidia hasara kutoka
kwenye mishahara yao wengine 4 wameshushwa vyeo na wengine 10 wamebadilishiwa
majukumu” alisema Jafo.
Aliongeza kuhusu MSM kupokea Fedha pungufu
ya Bajeti Iliyoidhinishwa ni kwa sababu Serikali hutegemea makusanyo ya mapato
kutoka vyanzo mbalimbali. Hivyo, kiasi kinachotumwa kwenye MSM hutegemea
mwenendo wa mapato yaliyopatikana lakini pia fedha za miradi ya maendeleo
zilizotolewa na Serikali kwa mwaka wa fedha uliotaguliwa 2016/17 zimeongezeka
ikilinganishwa na mwaka wa 2015/16.
Kwa mwaka
2016/17 fedha za miradi ya maendeleo zilizopokelewa na MSM ni Tsh. 705,927,921,596.20
sawa na 57% ya bajeti iliyoidhinishwa ya Tsh. 1,242,616,839,000 akati mwaka
2015/16, fedha zilizopokelewa zilikuwa
ni Tsh. 390,525,992,297 sawa 39% ya bajeti ya Tsh. 1,010,650,744,099.
Kuhusu changamoto katika Usimamizi wa Mapato
katika Mhe. Jafo alieleza Wizara imeendelea kuziba mianya ya uvujaji wa mapato
kwa kuhakikisha kuwa Halmashauri zinahamia katika matumizi ya mfumo wa
kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato ujulikanao kama Local Government Revenue
Collection and Information System (LGRCIS) ambapo takwimu zote za mapato
zinatunzwa katika mfumo huo ambao pia umeunganishwa na mashine za kukusanyia
mapato (Point of Sales) zinazotumiwa na Mawakala/Wakusanya mapato, na hivyo
kuiwezesha Halmashauri kufahamu mapato yaliyokusanywa na Wakala/Wakusanya mapato hao.
Vile vile, mfumo huo umeunganishwa na mifumo
ya benki, na hivyo kuwezesha Halmashauri kufahamu kiasi ambacho Wakala/Mkusanya
mapato amekiingiza kwenye akaunti ya benki ya Halmashauri ikilinganishwa na
kiasi alichokusanya.
Mpaka sasa, Halmashauri zote 185 tayari zimewekewa mfumo
huu wa LGRCIS
Wakati huo huo alieleza Kuhusu Vitabu 379
vya Kukusanyia Mapato ambavyo havikuwasilishwa kwa Wakaguzi amesema Licha ya kuwa idadi ya Halmashauri na idadi ya vitabu vya
kukusanyia mapato ambavyo havikuwasilishwa kwa Wakaguzi imepungua kutoka 871 katika Halmashauri 57 kwa mwaka 2015/16
mpaka vitabu 379 katika Halmashauri 21 kwa Mwaka 2016/17, OR – TAMISEMI
imeendelea kusimamia maelekezo ya Serikali ya Halmashauri zote ziachane na
ukusanyaji wa mapato kwa kutumia stakabadhi/vitabu vya kuandikwa kwa mkono, na
badala yake mapato yakusanywe kwa kutumia mashine za kielektroniki.
Waziri Jafo alimalizia kwa kutolea ufafanuzi
wa Soko la Mwanjelwa –Mbeya na kusema kuwa OR-TAMISEMI imeanza kuchukua hatua
kuhusiana na dosari mbalimbali zilizojitokeza katika ujenzi wa soko la
Mwanjelwa na kwa kuanza tulimuomba CAG kufanya ukaguzi maalum na taarifa
iliashiria makosa ya kijinai na tayari Serikali imelifikisha suala hili kwenye
vyombo vya Dola, ambapo pia Wahusika Wakuu wa mikataba husika na usimamizi wa
utekelezaji wake, nao pia wameshafikishwa kwenye vyombo vya Dola kwa ajili ya
uchunguzi na hatua zaidi. Serikali itaendelea kufanyia kazi mapendekezo
yaliyotolewa na CAG ili kuokoa hasara itokanayo na ujenzi wa soko hilo.
Hati Safi zimeongezeka katika Mamalaka za Serikali za Mitaa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 12, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment