Wazee 305 na walemavu 24 wa mji mdogo wa Mirerani wilayani
Simanjiro, wamepatiwa vitambulisho vitakavyowawezesha kupatiwa
matibabu bure na kuingia ndani ya migodi ya madini ya Tanzanite
Watu hao walikabidhiwa vitambulisho hivyo jana mtaa wa Kazamoyo
mji mdogo wa Mirerani na mkuu wa wilaya hiyo, Zephania Chaula.
Mwenyekiti wa sauti ya walemavu Mirerani, Robert Songa alisema
kundi hilo maalumu linapaswa kuangaliwa kwa jicho la huruma kwenye
sekta mbalimbali
Songa alisema kupitia vitambulisho hivyo, walemavu hao wataingia
ndani ya ukuta na kufanya shughuli zao, ikiwamo kuchekecha
mchanga wakati wa utafutaji wa madini ya Tanzanite
“Mkuu wa wilaya na ofisa madini mkazi Mirerani, Frederick Girenga
asanteni kwa kufanikisha sisi kupata vitambulisho hivi,” alisema
Songa
Naye Chaula alisema Serikali inawajali wazee na walemavu ndiyo
sababu wakawapa kipaumbele kwenye utoaji wa vitambulisho vya
kupata matibabu bure na kuingia ndani ya ukuta
Chaula alisema hiyo ni awamu ya kwanza, hivi sasa wanajipanga
kutoe kwa wazee na walemavu wengine ambao hawajavipata.
Wazee, walemavu wapewa vitambulisho bima ya afya, kuingia mgodi wa Tanzanite
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment