Kura kuamua mrithi wa Lissu TLS zapigwa

Wanachama wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) wameanza kupiga kura jijini Arusha leo, Aprili 14, 2018 kuwachagua viongozi watakaoongoza kwa kipindi cha mwaka mmoja

Katika uchaguzi huo atapatikana mrithi wa rais wa chama hicho, Tundu Lissu anayemaliza muda wake.
Wagombea wa nafasi ya urais ni Fatma Karume, Godwin Ngwilimi, Godwin Mwapongo na Godfrey Wesonga
Rugemeleza Nshalla anagombea nafasi ya makamu wa rais, huku nafasi ya mhazini ikiwaniwa na Nicholas Duhia
Uchaguzi huo pia unahusisha wajumbe wa baraza la uongozi lenye wajumbe saba.
Licha ya eneo la kupigia kura kuwa la wazi lakini kila mgombea ameweka mawakala wanaosimamia haki zao
Kura kuamua mrithi wa Lissu TLS zapigwa Kura kuamua mrithi wa Lissu TLS zapigwa Reviewed by KUSAGANEWS on April 14, 2018 Rating: 5

No comments: