RC GAMBO AFANYIWA DUA MAALUM KWA AJILI YA KUSAFIRI LEO KWENDA INDIA ILI KUREJESHA MWILI WA MAREHEMU MAMA YAKE MZAZI


Dua kwa ajili ya kumuombea mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambaye ameondoka nchini leo kuelekea India kwa ajili ya kufuata mwili wa marehemu mama yake Rehema Paulo Mumburi ili kurejesha nyumbani kwa ajili ya taratibu za maziko imefanyika nyumbani kwake jijini Arusha.

Dua hiyo ambayo imeongozwa na viongozi mbalimbali wa dini ya Kiislamu na Kikristo imehudhuriwa na Viongozi wa chama tawala,Wakuu wa ulinzi na usalama,wananchi pamoja na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema.

Wakizungumza katika Dua hiyo viongozi wa dini wamemtaka mkuu wa mkoa Mrisho Gambo kuwa na moyo wa uvumilivu na ampe mwenyezi Mungu nafasi mana ndiye aliyepanga hivyo kama wanadamu wanapaswa kushukuru.

Naye mbunge wa Arusha Godbless Lema amesema kuwa ni wakati wa kuendelea kuombea ndugu jamaa na marafiki wa familia ya Rc Gambo kwa kufiwa mama yao na anaposafiri kuelekea India Arudi salama

Mama Rehema Paulo Mumburi alifariki dunia huko nchini India alipokuwa akitibiwa katika hospitali ya Madras Medical Mission Chenai iliyipo Nchini India

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega Amesema kuwa Mrisho Gambo anaondoka saa kumi kupitia uwanja wa ndege wa KIA na anarajia kurejea na mwili wa marehemu Mama yake siku ya jumanne na atazikwa siku ya Alhamisi wiki ijayo Moshi mkoani Kilimanjaro.

RC GAMBO AFANYIWA DUA MAALUM KWA AJILI YA KUSAFIRI LEO KWENDA INDIA ILI KUREJESHA MWILI WA MAREHEMU MAMA YAKE MZAZI RC GAMBO AFANYIWA DUA MAALUM KWA AJILI YA KUSAFIRI LEO KWENDA INDIA ILI KUREJESHA MWILI WA MAREHEMU MAMA YAKE MZAZI Reviewed by KUSAGANEWS on April 14, 2018 Rating: 5

No comments: