Omar Ali Said ashinda tena urais ZLS


Wajumbe wa Chama cha Mawakili visiwani Zanzibar (ZLS), leo Aprili 14 wamemchagua tena Omar Ali Saidi Shaaban   kuwa Rais wa chama hicho kwa mhula mwingine wa pili

Uchaguzi hu umefanyika katika ukumbi wa jengo la Shirika la Bima, Unguja huku ukihudhuriwa na wajumbe wachache kutokana na kile kilichoitwa mwamko mdogo kwa mawakili visiwani hapa

Omar amechaguliwa bila kupingwa pamoja na katibu wake, Rajab Abdallah baada ya kuwa wanachama pekee waliojitokeza kugombea nafasi hizo ndani ya chama hicho

Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Rais huyo amesema kuchaguliwa kwake bila kupingwa kunaonyesha dhahiri mawakili visiwani Zanzibar wanamwamini na kukuubali uongozi wake
Amesema si kawaida sehemu yenye wasomi kwa kiwango cha wanasheria, wajumbe wengine kukataa kugombea lakini kwake imejitokeza na kwamba yote hayo ni kwa sababu wamekubali utendaji wake aliouita, uliotukuka

Amesema atahakikisha anasimamia misingi bora ya taaluma ya kisheria na kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu

“Nitahakikisha nasimamia na kutekeleza malengo ya chama hiki ili kila mtu anayestahiki kupatiwa haki za kisheria aweze kupata katika wakati mwafaka,” amese,a

Naye Rajab Abdallah amesema atahakikisha anatunza na kuheshimu uamuzi wa wajumbe wa chama hicho kwani anajua wapo wengi waliostahili
Omar Ali Said ashinda tena urais ZLS Omar Ali Said ashinda tena urais ZLS Reviewed by KUSAGANEWS on April 14, 2018 Rating: 5

No comments: