Mwanasheria mkongwe, Fatma Karume, ameshinda nafasi ya urais
wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS
Fatma, ambaye licha ya kuwa mwanachama wa TLS kwa muda
mrefu, lakini pia ni mtoto wa Rais wa sita wa Zanzibar, Amani Abeid Karume
Zoezi la kupiga na kuhesabu kura lilianza tangu asubuhi leo
Aprili 14, mjini Arusha na likakamilika jioni huku Fatma akiibuka na kura
820 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Wakili Godwin Ngwilimi, aliyepata kura
363
Wagombea wengine wa nafasi ya urais wa TLS walikuwa ni
Godwin Mwapongo aliyepata kura 12 na Godfrey Wasonga, aliyepata kura sita
Fatma Karume amezaliwa Juni 15, 1969, visiwani
Zanzibar,
Ni Mtoto wa rais wa sita wa Zanzibar, Amani Abeid Karume
Ni mjukuu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani
Karume
Ni mwanasheria katika kampuni ya uwakili ya IMMA Advocates
Ni mwanzilishi wa kampuni ya uwakili ya Karume and Co
Advocates 2004
Fatma amewahi kuwa mwanasheria wa mwanasiasa Tundu Lissu
katika kesi yake ya uchochezi, Julai mwaka jana
Ofisi za kampuni ya uwakili ya IMMMA zilizopo Upanga, jijini
hapa, ziliungua moto Agosti mwaka jana
BREAKING NEWS: FATMA KARUME ASHINDA URAIS WA TANGANYIKA LAW SOCIETY (TLS)
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment