Watu saba washikiliwa mkoani Tabora

 Watu saba wakiwamo waganga wawili wa jadi, wanashikiliwa na polisi wilayani Igunga mkoani hapa kwa tuhuma za kupiga ramli na kusababisha famila tatu kukosa makazi baada ya nyumba zao kuteketezwa kwa tuhuma za kishirikina

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Wilbrod Mutafungwa amewataja waganga hao kuwa ni Chemani Ndishiwa (79) na Nzali Mayunga (40

Wengine waliokamatwa ni Masanja Seni (65), Kasura Msomi (31), Michael James (19), Dotto Lukelesha (41) na Samwel  Jonas (18) wote wakazi wa kijiji cha Mwakwangu

Mutafungwa amesema tukio hilo lilitokea jana Aprili 28, 2018 saa tano usiku katika kijiji hicho baadhi ya wananchi walikwenda kwa waganga hao wawili kupiga ramli na kuambiwa kijijini wapo baadhi ya familia ni wachawi

Amesema baada ya kuelezwa hivyo, baadhi wa wananchi waliamua kukodi vijana kwa kuwalipa fedha na hakuweza kutaja kiwango waliokwenda kwenye nyumba ya Luli Lukeresha na kuichoma

“Baada ya kufanya unyama huo, vijana hao walikwenda tena katika miji mingine ambayo waliichoma na kutoweka ingawa  wananchi walitoa taarifa polisi Igunga,” amesema




Watu saba washikiliwa mkoani Tabora Watu saba washikiliwa mkoani Tabora Reviewed by KUSAGANEWS on April 29, 2018 Rating: 5

No comments: