Rais John Magufuli amewataka wanakijiji cha
Migori mkoani Iringa kutumia barabara ya lami ya Iringa-Dodoma kujitajirisha
Akizungumza leo Jumapili Aprili 29,
aliposimama kwa muda katika kijiji cha Migori wakati akielekea Iringa, Rais
Magufuli amewataka wanakijiji hao kuchapa kazi
“Barabara imekamilika mnaiona, itumieni ili
mtajirike, limeni mazao kwa bidii na msafirishe kwenda sehemu mbalimbali za
nchi,” amesema Rais Magufuli
Aliwataka kutumia mvua zinazoendelea, kulima
na kufuga ili waweze kunufaika
Rais Magufuli atakuwa na ziara mkoani Iringa
ambako Jumanne Mei mosi atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za Siku ya
Wafanyakazi Duniani zitakazofanyika kitaifa mkoani Iringa
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza
amesema sherehe hizo zitahudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai, mawaziri na wabunge.
Rais Magufuli awataka Iringa kutumia barabara ya lami
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 29, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 29, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment