Kifo mdogo wa Heche ngoma nzito

Uongozi wa Serikali na Polisi mkoani Mara, wanafanya mashauriano na familia ya Suguta Marwa, ndugu wa mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche anayedaiwa kuuawa na polisi kwa kuchomwa kisu usiku wa kuamkia Aprili 27

Majadiliano hayo yanaendelea huku kamanda wa polisi Kanda Maalumu  Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe akitangaza askari anayetuhumiwa kufanya mauaji hayo, E.1156 Koplo William Marwa kushikiliwa kwa mahojiano

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima juzi Aprili 27, 2018 alitembelea familia ya marehemu na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa ili haki itendeke

“Hakuna mtu aliye juu ya sheria hata ningekuwa mimi Adam Malima, mkuu wa mkoa ndiye ningefanya jambo hili ningechukuliwa hatua za kisheria. Haki ya marehemu lazima ipatikane,” amesema Malima

Licha ya kuitembelea familia kuhani msiba akiwa ameongoza na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, Malima alitembelea Kituo cha Polisi Sirari na chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Wilaya ya Tarime ulikohifadhiwa mwili wa Suguta tangu juzi

Msemaji wa familia, Philemon Suguta amesema vikao kati yao na Serikali kuhusu msiba huo vitafanyika baada ya baadhi ya ndugu akiwamo mbunge Heche ambao wapo njia kwenda Tarime kuwasili

“Jambo la msingi kwa familia ni hatua za kisheria kuchukuliwa, haiwezekani mtuhumiwa aliyekamatwa akiwa hai afie mikononi mwa polisi, tena kwa kuchomwa kisu,” amesema Suguta
Baba mgogo wa marehemu, Issa Suguta aliwatuhumu polisi waliomkamata ndugu yake kumpiga hadi kumjeruhi kabla ya kummalizia kwa kumchoma kisu

Naye katibu wa Chadema mkoa wa Mara, Chacha Heche ambaye ni ndugu wa marehemu Suguta amesema hadi sasa, familia inaamini mauaji hayo ni uhalifu usiohusiana na masuala ya kisiasa



Kifo mdogo wa Heche ngoma nzito Kifo mdogo wa Heche ngoma nzito Reviewed by KUSAGANEWS on April 29, 2018 Rating: 5

No comments: