Rais Magufuli asema hakula nyama mwezi mmoja akiwa Iringa

Rais John Magufuli amefika Iringa na kusimulia mara ya kwanza alipopelekwa mkoani humo kusoma kwamba hakula nyama kwa mwezi mmoja baada ya kutahadharishwa na watu kuwa akifika asile kitoweo hicho.
Akihutubia wakazi wa Iringa wakati wa ufunguzi wa barabara ya Iringa-Fufu leo Aprili 29, 2018; Rais Magufuli amesema alifika Iringa kwa mara ya kwanza mwaka 1978/79 kwa ajili ya masomo katika Sekondari ya Mkwawa
“Niliambiwa usile nyama, usile mshikaki Iringa na kweli sikula," amsema na kwamba, baada ya kukaa muda alibaini wakazi wa Iringa hasa wanaume kuwa ni wakarimu
"Wanaume wa Iringa ni wapole sana, unamchokoza lakini anajinyonga yeye badala ya kukuadhibu wewe," ameongeza Rais Magufuli huku akishangiliwa na umati wa wananchi
Anasema watu wa Iringa ni tofauti na wenzao wa mkoani Mara ambao ukiwachokoza utakiona cha mtema kuni
Rais Magufuli asema hakula nyama mwezi mmoja akiwa Iringa Rais Magufuli asema hakula nyama mwezi mmoja akiwa Iringa Reviewed by KUSAGANEWS on April 29, 2018 Rating: 5

No comments: