Tabora. Watoto wa kike 5,913,
wenye umri chini ya miaka 18 mkoani Tabora, wamebainika kupata ujauzito
katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu
Kauli hiyo imetolewa leo mjini
hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifungua semina ya siku
moja ya Kamati ya Huduma ya Afya ya Msingi ya Mkoa huo
Akizungumza leo Aprili 20 katika
semina hiyo, Mwanri amesema: “Takwimu hizo zinasikitisha na zinaonyesha
kuwa bado kuna tatizo kubwa la watu wazima kukatisha ndoto za watoto wa kike
mkoani humo.”
Mwanri amesema Halmashauri ya
Wilaya ya Nzega, inaongoza kwa wasichana 1,438 wenye umri wa chini ya miaka
18, kupata mimba
Nyingine ni Igunga (995) Kaliua
(894), Sikonge (743) Uyui (640), Urambo (630), Manispaa ya Tabora (530) na
Nzega Mjini (49)
Amesema vitendo hivyo si tu
vinarudisha nyuma maendeleo ya watoto bali vinawaweka katika hatari ya kupata
saratani ya mlango wa kizazi kwa kuwa wanashiriki ngono katika umri mdogo
Mwanri amewaagiza viongozi na
watendaji katika Mkoa wa Tabora kuwafuatilia na kuwachukulia hatua haraka
watu wote waliohusika na ujauzito wa watoto hao ili waweze kufikishwa katika
vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazowakabili.
|
Wasichana 5,900 wa umri chini ya miaka 18 wapachikwa mimba Tabora
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment