ASKOFU Mkuu wa Kanisa la InternationalEvangelism lililopo Sakila ,wilayani Arumeru,mkoani Hapa ,Elihudi Isangya (69) anashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani hapa Kwa tuhuma za Mauaji ya
kaka yake.
Wengine wanaoshikiliwa ni mdogo wake na Askofu aitwaye,NdewarioIsangya (59) pamoja na Afisa mwandamizi wa kanisa hilo,Obadia Nanyaro(60)wote wakazi wa Sakila wilayani humo.
Watuhumiwa hao Kwa pamoja walikamatwa juzi majira ya Saa 1.30 Usiku katika kijiji cha sakila wakihusishwa na tukio la mauaji ya marehemu Nixon Isangya(71) ambaye aliuawa nyumbani Kwake Moivaro kwa kupigwa na kitu chenye ncha Kali kichwaji januari 8 mwaka 2017.
Kaimu kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani hapa Yusufu Ilembo amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa alikamatwa na baada ya kuhojiwa aliwataja watuhumiwa hao wanaodaiwa kuratibu mpango huo.
Ilembo alisema kuwa Polisi wanaendelea na uchungu wa tukio hilo na pindi utakapokamilika wahusika watafikishwa mahakamani
Akizungumzia tukio hilo mtoto wa Marehemu Nixon, aitwaye Jeny Nixon Isangya ameeleza kuwa baba yake aliuawa nyumbani kwake wakati huo alikuwa akiishi na Kijana mmoja aliyemtaja Kwa jina la Simon
Kaaya ,.
Hata hivyo baada ya tukio hilo Kijana huyo alitoweka nyumbani hapohadi alipokamatwa juzi siku nyumbani kwake baada ya wananchi kuizingira nyumba yake na kumfikisha kituo cha
Polisi
"Huyu Kijana alienda kumwomba Marehemu baba yangu aishi naye akidai anamwonea huruma kumwona akiishi peke yake " Amesema
Ameongeza kuwa Kijana huyo aliweza kuishi
na Marehemu kuanzia januari mosi mwaka Jana kabla ya kuuawa januari 8
na kukutwa mwili wake umelazwa kitandani na kufunikwa shuka huku akiwa na
jereha kichwani
Hata hivyo amedai kuwa katika
uhai wake marehemu baba yake alikuwa na mgogoro wa muda mrefu na Askofu Isangya kiasi cha kutosemeshana
"Ugomvi wa baba yangu na baba Askofu Isangya ni wa muda mrefu walikuwa hawaongei hadi Marehemu alipokutwa Ameuawa kikatili chumbani kwake" Amesema
Katika hatua nyingine jana
majira ya saa sita usiku Askofu alifanikiwa kuachiwa huru Kwa
dhamana huku watuhumiwa wenzake wakibaki mahabusu
Hata hivyo Askofu huyo amekamatwa tena mapema Leo na kurejeshwa mahabusu katika kituo kikuu cha
Polisi jijini hapa wakati akisubiri taratibu za kiupelelezi
Askofu Isangya kwa kumuuwa ndugu yake.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment