Msanii wa filamu bongo
Rammy Galis ambaye alishawahi kuwa kwenye mahusiano na Agnes Masogange
aliyefariki hapo jana, ametoa siri ambayo wengi walikuwa hawaijui kuhusu maisha
ya Agnes.
Kwenye ukurasa wake wa instagram
Rammy Galis ameandika ujumbe akionesha kuhuzunishwa na kifo cha mrembo huyo
ambaye alibarikiwa na Muumba kwa urembo wake, na kusema kwamba walipokuwa
kwenye mahusiano aliwahi kucheza filamu yake ambayo kama ilitabiri kifo chake,
kwa kuigiza kufa mwisho wa kisa hiko kilichopewa jina la 'hukumu'.
“Tulikesha usiku na mchana ili
ucheze filamu yetu kwa hisia, ukasema hii iwe kumbukumbu yako kama niliwahii
hata kwenye kazi zako kukusaidia, sasa kwanini filamu yetu tulitunga jina
liitwe #hukumu?
ilikuwaje story ya filamu mwisho unafariki? kwani tulikua tunatungia iwe kweli hukumu yako? Mungu ndio hakimu wa viumbe vyote katika dunia , umeondoka ghafla sanaa , na hii pia ni funzo umeniachia”, ameandika Rammy Galis akiambatanisha picha ya wawili hao pamoja.
Kutokana na kauli hii ya Rammy
Galis, tunaweza sema Masogange naye amepitia kifo ambacho muigizaji nguli wa
filamu za bongo Steven Kanumba alifariki, kwa kuigiza kifo kwenye filamu yake ya
mwisho, na kweli kabla ya filamu kutoka alipatwa na mauti.
Aliyekuwa mpenzi wa Masogange, afunguka siri kubwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment