Mbunge Tundu Lissu Amesema
sheria ya uendeshaji wa Bunge halijaweka masharti yeyote ya kupatiwa fedha za
matibabu kama alivyo tangaza Spika wa Bunge Job Ndugai hivi karibuni na wala
hakuna kifungu chochote kinachozungumzia kibali cha Hospitali ya Muhimbili au
cha Rais Magufuli.
Lissu amebainisha hayo usiku wa
kuamkia leo kupitia ukurasa wa kijamii zikiwa zimepita takribani siku tatu
tokea Spika wa Bunge, Job Ndugai kutoa ufafanuzi juu ya matibabu ya Mbunge huyo
kuwa Bunge haliwezi kuidhinisha fedha kwa ajili ya matibabu yake kwa kuwa
halijapata vibali vitatu ambavyo vingemuwezesha kupata fedha za matibabu kutoka
Bungeni.
"Ukweli ni kwamba kauli ya
Spika Ndugai inathibitisha jinsi ambavyo Bunge limepoteza mamlaka na hadhi yake
chini ya uongozi wake dhaifu. Hata masuala ambayo Sheria haijampa Rais mamlaka,
Spika Ndugai ameyakabidhi. Kauli hiyo ni uthibitisho pia wa jinsi ambavyo Bunge
linaendeshwa bila kufuata sheria, kwa chuki na upendeleo wa kisiasa", amesema Lissu.
Pamoja na hayo, Lissu ameendelea kwa
kusema "yeye amekwenda India mara nyingi kutibiwa kabla na
baada ya kuwa Spika kwa gharama za Bunge. Mimi mbaya wao niliyepigwa risasi
nikiwa nahudhuria vikao vya Bunge ninakataliwa matibabu kwa sababu zisizokuwa
na msingi wowote. Sio kweli kwamba sikufuata utaratibu, kama maana ya neno hilo
ni utaratibu uliowekwa na sheria".
Lissu ameendelea kusema..
"Kusema nisubiri kibali cha
Bunge au cha Muhimbili au cha Rais Magufuli ilikuwa ni kunitakia kifo cha wazi.
Katika mazingira ya jaribio la mauaji dhidi yangu, utaratibu pekee uliokuwa unawezekana ulikuwa ni kunihamisha nchini kwa dharura. Nilikuwa nimeumizwa vibaya, mifupa imevunjwa kila mahali, nimepoteza damu nyingi na risasi zimejaa tumboni. Kusema nisubiri kibali cha Bunge au cha Muhimbili au cha Rais Magufuli ilikuwa ni kunitakia kifo cha wazi".
Katika mazingira ya jaribio la mauaji dhidi yangu, utaratibu pekee uliokuwa unawezekana ulikuwa ni kunihamisha nchini kwa dharura. Nilikuwa nimeumizwa vibaya, mifupa imevunjwa kila mahali, nimepoteza damu nyingi na risasi zimejaa tumboni. Kusema nisubiri kibali cha Bunge au cha Muhimbili au cha Rais Magufuli ilikuwa ni kunitakia kifo cha wazi".
Aidha, Lissu amedai uamuzi wa yeye
kupelekwa Nairobi nchini Kenya umetokana na makubaliano ya kikao kilichofanyika
Hospitali ya Mkoa wa Dodoma ambapo Spika Ndugai na Naibu wake walikuwepo kwenye
kikao hicho pamoja na viongozi wengine wa nchi akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani
Mwigulu Nchemba, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na Katibu Mkuu wake Dkt.
Ulisubisya Mpoki na Mwenyekiti Mbowe na wabunge kadhaa walihudhuria pia.
"Baada
ya kukubaliana kwamba napelekwa Nairobi, ndege ililetwa Dodoma saa sita za
usiku. Uwanja wa Ndege wa Dodoma hauruhusu ndege kuruka au kutua baada ya saa
12 jioni. Nani aliyeruhusu ndege iliyonichukua kutua na kuruka saa sita usiku
kama hakukuwa na kibali cha Bunge?", amehoji Lissu.
Sakata la matibabu Lissu amvaa Spika wa Bunge Job Ndugai
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment