Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga
amesema, jalada la kesi ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha
Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini amelifunga rasmi
Hayo ameyasema leo Aprili 20, 2018; Ikulu
jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari huku akionya watu
wanaovunjua amani kutofumbiwa macho wakiwamo waandishi wa habari
Amesema jeshi la polisi linapotumia nguvu
kuzuia maandamano, haliwezi kushtakiwa au hata kukitokea vurugu na kusababisha
mauaji huwezi kulishtaki jeshi
”Katika maandamano yale ya watu zaidi ya
200, huwezi kubaini nani amehusika na kumpiga risasi Akwilina na mwili wake
haukutolewa risasi yoyote
Alipoulizwa kuhusu askari waliokamatwa baada
ya kutokea kwa tukio hilo, Biswalo amesema, “kama jalada nimelifunga, kwa hiyo
askari wale nao wameachiwa huru hawana hatia.”
Mkurugenzi huyo amesema moja ya jukumu lake
ni kuhakikisha amani inakuwapo,”na niseme tu kuwa, mimi sina chama cha siasa,
si mwanasiasa, kwa hiyo sitamvumilia mtu awe mkubwa wala mdogo,
nitamshughulikia.”
“Na wanaosema wataandamana, waambieni
wasifanye hivyo kwani wakiandamana watakwenda kuwasilimulia familia yake,”
amesisitiza Biswalo
Pia, amevionya vyombo vya habari ambavyo
vinavyoweza kuchangia uvunjifu wa amani, hatua zitachukuliwa hivyo kuvitaka
kuwa makini na kutimiza wajibu wao kwa kufuata misingi ya taaluma yao
Jalada kesi ya mauaji ya Akwilina lafungwa na DPP
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment