|
Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kati ya wanawake 480 waliozungumza na
wanasheria jana Jumatatu Aprili 9, 2018, 61 wamezalishwa na kutelekezwa na
wabunge pamoja na viongozi wa dini
Makonda ametoa kauli hiyo leo Aprili 10, 2018 wakati
akitoa salamu zake kwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi
wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka
14 unaofanyika leo katika viwanja vya Zakeem Mbagala
Amesema wanawake 47 wanadai wabunge ndio
wamewatelekeza na 14 wamesema kuwa wamezalishwa na kutelekezwa na viongozi wa
dini
"Katika Mkoa wangu wa Dar es Salaam, mwaka 2017
wanawake waliojifungua walikuwa 129,347 na kati ya hao asilimia 60
walitelekezwa na watoto 274 waliokotwa maeneo mbalimbali ndiyo maana tumeona
tuje na mkakati huu kuhakikisha tunapambana na wale wanaume wote
wanaotelekeza watoto," amesema Makonda
|
Wanawake 61 Dar wadai kuzaa na viongozi wa dini, wabunge
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 10, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment