Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amefunguka na kuwataka
baadhi ya Wabunge Bungeni kuacha kuwatetea wasanii wanaoimba nyimbo zisizokuwa
na maadili kwa kuwa kufanya hivyo kuna pelekea kuonekana taifa la Tanzania kuwa
mfu lisilokuwa na utamaduni wake.
Waziri Mwakyembe ametoa kauli hiyo
leo (Aprili 10, 2018) kwenye mkutano wa 11 kikao cha sita kinachoendelea
kufanyika mkoani Dodoma wakati akijibu swali la Nyongeza kutoka kwa Mbunge
Catherine Magige ambaye alitaka kufahamu ni kwanini kamati ya maudhui
inashindwa kufanya kazi zake kwa wakati mpaka inafikia muda wasanii wanaachia
kazi zao za sanaa ndio wao wanaibuka na kuanza kuwafungia kazi hizo, je
wameshindwa kazi ?.
"Kila taifa lina utamaduni wake
na lazima liulinde kwa udi na uvumba, tunachokifanya sisi sio kwamba tuna vita
na wasanii wetu, hapana. Lakini lengo letu ni kulinda maadili ambayo katika
kipindi hiki cha utandawazi kumekuwepo na mmong'onyoko mkubwa katika taifa letu
na lazima tuchukue hatua. Tunachokifanya sisi hapa sio jambo jipya duniani,
kila mtu anafanya hivyo na hawa wasanii wetu tumeshawasamehe wasirudie
tena", amesema Dkt. Mwakyembe.
Pamoja na hayo, Waziri Mwakyembe
ameendelea kwa kusema kwa kutumia baadhi ya nukuu ya Hayati Baba wa Taifa
Julius Kambarage Nyerere kwamba "Taifa lisilokuwa na utamaduni
wake ni taifa mfu'. Sisi hatuwezi kukubali kuwa taifa mfu. Yanayotokea Tanzania
yanatokea duniani kote".
Kwa upande mwingine, Waziri
Mwakyembe amesema Wizara yake kupitia kamati ya maudhui itaendelea kuzifungia
nyimbo zisizokuwa na maadili ili waweze kulinda utamaduni wa taifa la Tanzania.
Waziri Mwakyembe tutaendelea kufungia wasanii
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 10, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment