Mke, mume wakutana kwa Makonda


Mapya yameendelea kuibuka katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya wazazi wawili kukutana ana kwa ana katika ofisi hizo

Kuanzia jana asubuhi, wanawake waliotelekezwa na wenza wao walifurika katika ofisi ya RC Makonda kama alivyoagiza ili kuwasaidia kisheria

Katika tukio la leo, Aprili 10, mwanamke, Sylvia Felisiano alitinga katika viwanja vya ofisi ya RC Makonda, baada ya kusikia mume wake amekwenda kulalamika kuwa amemkimbia na watoto wao watatu

Awali, mwanaume, Tito Chembs, alifika kwa mkuu wa mkoa akilalamika kuwa mke wake amempokonya watoto na kwenda nao Bukoba

Saa chache baadaye, Sylvia alipata taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii na kutinga katika ofisi hizo

Maofisa ustawi wa jamii waliokuwa wakisikiliza mashauri hayo, waliwachukua wenza hao na kuingia nao ndani, huku Sylvia akionekana mwenye hasira na kuahidi ataongea kwa kina na wanahabari

Mke, mume wakutana kwa Makonda Mke, mume wakutana kwa Makonda Reviewed by KUSAGANEWS on April 10, 2018 Rating: 5

No comments: