Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda amewataka wanawake waliotelekezewa watoto kuwa na moyo wa
uvumilivu katika kipindi cha mvua ili mradi kila mtoto apatiwe haki yake
inayostahili kama alivyoahidi japokuwa anajua kuna wanaume wanaomba dua mvua
iendelee kunyesha ili mambo yaharibike
Paul Makonda ametoa kauli hiyo leo
Aprili 13, 2018 alipokuwa akizungumza na umati mkubwa wa mama ambao mpaka sasa
hawajafanikiwa kupata namba ya kuingia ndani kusikilizwa shida zao na kuwasii
wamama hao kuwa na subira wapatiwe namba ili zoezi hilo liweze kuendelea
kusudi kila mmoja apate haki yake.
"Furaha niliyonayo nikuona kuna
watu wameshaanza kupata amani ya mioyo yao na hilo ndio lilikuwa lengo kubwa la
serikali yenu na watumishi hawa waliojitolea ambako kiukweli siwalipi hata
senti 5. Lakini zaidi ya yote ndio lengo la Mungu kuleta amani katika familia.
Leo ni siku ya Ijumaa ambayo ilikuwa ya mwisho lakini ukitazama kuna watu hata
namba hawajapata lakini kuna mambo mawili lazima muyapate", amesema Makonda.
Pamoja na hayo, Makonda ameendelea
kwa kusema "jambo la kwanza ni lazima kila mtoto apate kile
anachostahili, jingine ni kupata bima ya afya niliyoahidi kwa kila mtoto
aliyekanyaga katika viwanja hivi. Kwasababu hizo niwaombe muwe wavumilivu leo
wote ambao hamjapewa namba mtapewa. Vumilie mvua najua wakina baba huko walipo
wanaombea mvua iendelee kunyesha ili mambo yaharibike lakin waambieni kama
mliweze kuvumilia miezi tisa na matusi yote waliyowatukana sembuse mvua ? kwa
hiyo tutaendelea kuvumilia mpaka haki itakapopatikana".
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Paul Makonda amesema mpaka kufikia siku ya tano leo
wameshasikilizwa takribani wamama 4,000 huku familia 205 kwa hesabu za siku ya
jana (Alhamisi) yaani watoto 205 wameondokana na mfumo wa omba omba na sasa
wanapatiwa huduma zote zinazostahili kwa baba na mama zao wakiwa pamoja.
"Wanaombea mambo yaharibike"- Makonda
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 13, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment