TMA yatoa tahadhari kubwa


Mamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo yote ya pwani kuanzia leo usiku mpaka Aprili 16 mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo jioni ya leo (Ijumaa) na kudai kutakuwepo vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 katika saa 24 ambavyo vinatarajiwa katika maeneo ya mkoa wa Tanga, Dar es Salaam, Morogoro, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Aidha, TMA imewashauri wakazi wa maeneo yaliyotajwa kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zinazotolewa.

Kwa taarifa kamili angalia hapa chini
      


TMA yatoa tahadhari kubwa TMA yatoa tahadhari kubwa   Reviewed by KUSAGANEWS on April 13, 2018 Rating: 5

No comments: