Hukumu ya kesi ya Tito Machibya
(maarufu Nabii Tito), ambayo ilikuwa itolewe uamuzi jana, iliahirishwa hadi
Aprili 20, mwaka huu kutokana na hakimu anayehusika na kesi hiyo kuwa na
dharura.
Akitoa maelezo mahakamani hapo,
Mwanasheria wa Serikali Judith Mwakyusa, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama
ya Wilaya, Godfrey Pius, alisema kesi hiyo ilikuja mahakamani hapo kwa ajili ya
kutolewa uamuzi mdogo.
Mwakyusa alisema kesi hiyo ilikuwa
itolewe uamuzi jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya
Dodoma, James Karayemaha, lakini amepata dharura.
“Mheshimiwa Hakimu shauri hili
limeletwa kwako kwa ajili ya kuahirishwa kutokana na Karayemaha kuwa na
dharura,” alisema.Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Godfrey Pius, aliahirisha
kesi hiyo hadi Aprili 20, mwaka huu itakapoletwa tena kwa ajili ya uamuzi.
Pius alisema mtuhumiwa atarudishwa
rumande hadi tarehe hiyo.
Aprili 5, mwaka huu Hakimu
Karayemaha alisema wamepokea taarifa ya kitabibu kutoka taasisi ya magonjwa ya
akili ya Isanga inayomhusu Mchibya na uamuzi ungetolewa jana.
Nabii Tito alidai ana matatizo ya
akili yaliyosababisha kutaka kujiua na kuiomba mahakama kuamuru akachukuliwe
vipimo ili kupata uhakika wa afya yake ya akili.
Katika kesi hiyo, anashtakiwa kwa
kosa la kutaka kujiua kwa kujikata na wembe na kujijeruhi kwenye maeneo ya
tumbo, Januari 25, mwaka huu katika mtaa huo wa Ng’ong’ona alipokwenda
kukamatwa na polisi.
Hukumu ya Nabii Tito Kutolewa April 20
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment