Mapadri watatu wa Kanisa Katoliki
Jimbo la Same, wamefariki dunia ndani ya saa 72. Kanisa limesema vifo vya aina
hiyo havijawahi kutokea.
Waliofariki wametajwa kuwa ni Padre
Ubaldus Kidavuri, Padre Arbogast Mndeme na Michael Kiraghenja, wote wa jimbo
hilo. Wawili kati ya hao walifariki ghafla usingizini.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani
ya kanisa hilo, padre mmoja ndiye aliyekuwa akiumwa na alifariki akiwa katika
Hospitali ya KCMC.
Taarifa ya vifo vyao ilitolewa jana
na Askofu wa Jimbo la Same, Mhashamu Rogath Kimario.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mapadri
hao wanatarajiwa kuzikwa Aprili 17, katika Makaburi ya Mapadri Jimbo la Same.
Taarifa ilisema haijawahi kutokea
vifo vitatu vilivyopishana kwa saa 24 katika jimbo moja.
“Jana nilionana na Padri Kidavuri na
alikuwa akijiandaa kwa safari ya kwenda kuzika wenzie na nikampa pole pale St.
Joseph, alikuwa mzima wa afya. Wapumzike kwa amani, amina,” alisema Padre
Kimario.
Akithibitisha vifo hivyo jana,
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Raymond Saba,
alisema kanisa limepokea kwa mshtuko mkubwa kufuatia vifo hivyo vya ghafla.
“Vifo vimetushtua sana maana
vimekuwa vya ghafla mno, tulikuwa nao na walikuwa wazima kabisa,” alisema Padre
Saba.
Alisema wanatarajia mazishi yatafanyika
Jumanne ijayo, Same.
Mapadri Watatu Wafariki Dunia Ghafla
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment