Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangala, amezitaka halmashauri
zote nchini kuacha kupora maeneo ya hifadhi za misitu kwa kisingizio cha
kilimo.
Rai
hiyo aliitoa jana wakati akifungua mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi
wa Wakala wa huduma za misitu Tanzania, uliofanyika mkoani hapa jana.
Dk.
Kigwangala alisema halmashauri zote nchini zinatakiwa kuacha mara moja
kuvamia na kupora maeneo ya hifadhi ya misitu kwa kisingizio cha uhitaji
wa maeneo ya kilimo.
“Kuna
baadhi ya halmashauri za mikoa ya Pwani zimewapa wawakezaji eneo la
kilimo ndani ya msitu wa hifadhi na matokeo yake mwekezaji amekuwa
akivuna misitu yetu,” alisema Dk. Kigwangala.
Aliagiza wakala wa huduma za misitu nchini kuhakikisha wanalisimamia agizo hilo.
Hata
hivyo, alisema matumizi ya mkaa na kuni ni changamoto kubwa kwa
uharibifu wa misitu nchini kutokana na watu wengi kutegemea nishati hiyo
kwa matumizi ya nyumbani.
Kutokana na matumizi ya mkaa na kuni, inakadiriwa kuwa hekta 400,000 hadi 1,000,000 zinateketea kila mwaka.
Dk.
Kigwangala alisema mabaraza ya wafanyakazi yanasaidia kuleta tija kwa
watumishi wake mahali pa kazi na kupitia kikao hicho, waangalie mambo
muhimu ya kujadiliana ili kupata majibu ya changamoto za kiofisi.
Aidha, aliwataka wakala wa misitu nchini kuhakikisha wanasimamia kujua idadi ya miti inayopandwa katika maneo mbalimbali.
“Hivi
katika kampeni hizi za upandaji miti zilizoanzishwa na Makamu wa Rais,
Samia Suluhu Hassan, mnaijua idadi yake kweli, mnajua miti mingapi
ilikufa na iliyobaki ni mingapi? Naomba mhakikishe mnakuwa na hizo
takwimu,” alisisitza Dk. Kigwangala.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dosantos
Silayo, alisema jumla ya misitu 11 itahifadhiwa katika mwaka huu wa
fedha katika wilaya za Chunya, Singida, Chamwino na Handeni.
Alizitaja
wilaya zingine kuwa ni Nyasa, Buhigwe, Tunduru na Mkinga, lengo likiwa
ni kuhifadhi bioanuai na mapito ya wanyama pori na hifadhi za maji.
Hata
hivyo, alisema watumishi wa wakala huduma za misitu wanakabiliwa na
changamoto za kujeruhiwa na wengine kupoteza maisha kutokana na
kushambuliwa na majangili wanapokuwa kwenye doria za kutekeleza majukumu
yao.
Alisema,
kuna vijiji 228 vilivyoingia katika maeneo ya hifadhi nchini, lakini
wanaendelea kuzungumza na wahusika ili kutatua migogoro hiyo.
Prof.
Silaya alizitaja changamoto zingine kuwa ni uvamizi wa misitu kwa
shughuli mbalimbali za kibinadamu pamoja na usafirishaji haramu wa mazao
ya misitu unatishia uwepo wa rasilimali hiyo kwa vizazi vijavyo.
Kigwangala azionya halmashauri
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment