Jumla ya lita 164 za damu zimepatikana katika
wilaya ya Ngara mkoani Kagera baada ya wananchi wengi kujitokeza kuchangia damu
kwa hiari
Lengo la kuchangia damu hiyo imedaiwa kwamba ni kusaidia
wagonjwa walioko katika hospitali za Nyamiaga, Murugwanza na Rulenge
wanaohitaji huduma hiyo
Mratibu wa maabara na damu salama wilayani
Ngara Mugisha Lubagola ametoa taarifa hizo leo Aprili 8 baada ya zoezi
hilo kufanyika katika uwanja wa michezo wa kokoto ambapo uhamasishaji wa
kuchangia damu umefanywa na Radio Kwizera mjini Ngara kupitia Kipindi cha
Asubuhi njema
Lubagola amesema damu hiyo itasaidia wagonjwa wanaopata
ajali, watoto wachanga, na akina mama wanaojifungua wakiwemo wa upasuaji katika
hospitali hizo japo haiwezi kukidhi mahitaji kwa mwezi katika
Hospitali na vituo vya Afya
Amesema wilaya hiyo inahitaji lita 290 kila mwezi
lakini zinazopatikana kwa watu kuchangia damu ni kati ya lita 70 mpaka 85
Amesema wanalazimika kwenda kuazima damu kutoka wilaya jirani za
Karagwe , Biharamulo na Misenyi
“Watu wanahitaji damu kutokana na mwili kushindwa kutengeneza
chembechembe nyekundu za damu, ambayo kazi yake ni kusafirisha Oksijeni na
kuweza kufanya kazi kuendelea kupumua na kuishi”Amesema Lubagol
Amesema binadamu ili amchangie mwenzake damu lazima awe na
umri wa miaka 18 mpaka 65 na achangie kila baada ya miezi mitatu, awe na afya
bila kuwa na magonjwa kama kisukari ambapo siku ya kutoa damu asiwe na
ugonjwa wa shinikizo la damu (presha
Aidha Kaimu mratibu wa uhamazishaji na
mwendeshaji wa kipindi cha Asubuhi njema Radio Kwizera Boazi Zobanya, amesema
mwaka jana ulifanyika utafiti mikoa sita ya kanda ya
ziwa yenye watu milioni 10, wanatakiwa kutumia unit 110,000
Zobanya amesema kwa mwaka jana baada ya kufanya
utafiti katika mikoa ya Kagera, Kigoma Geita, Mwanza,
Mara Shinyanga Simiyu na Tabora ilibainika ukusanyaji wa damu
ulikuwa lita lita 51,000 sawa na asilimia 40 ya mahitaji
“Ilitajwa ufinyu wa bajeti na watu kutoelimishwa
kuhusu umuhimu wa kuchangia damu ni miongoni mwa changamoto zinazosababisha kuwepo
kwa vifo vingi vinavyotokea kutokana na uhaba wa damu”amesema
Zobanya.
“Damu tunayoipata inapelekwa kwenye maabara ya vipimo
vya Hospitali ya Bugando na kubaini Makundi ya kumpatia
mgonjwa kwa maana kila mtu analo kundi la damu linalomstahili kwenye
mwili”Amesema
Wananchi wachangia lita 164 za damu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 08, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment