Vijana watatu waliotoweka Pemba wapatikana


Watu watatu kati ya sita waliotoweka katika mazingira ya kutatanisha usiku wa kuamkia Ijumaa Aprili 6, 2018 katika Kijiji cha Mitambuuni shehia ya Mtambwe, Mkoa wa Kaskazini Pemba wameonekana alfajiri ya leo Jumapili Aprili 8, 2018

Wameonekana katika Kijiji cha Mkungu Jimbo la Mtambile wilayani Mkoani

Akizungumza kamanda wa polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Sheikhan Mohamed Sheikhan amethibitisha kupatikana kwa watu

Amewataja vijana waliopatikana kuwa ni Said Shanani Mohamed (16), Juma Kombo Fimbo (17) na Abdallah Khamis Abdallah (19

Imeelezwa vijana hao walionekana alfajiri, wawili kati yao mikononi wakiwa na kamba

Amesema taarifa zaidi itatolewa baadaye na kamanda wa Mkoa wa Kaskazini ambako ndiko walikotoweka

“Kwa sasa jeshi linafanya kazi na taarifa rasmi itatolewa kwenu na jamii kwa jumla hapo baadaye,’’ amesema kamanda Sheikhan

Amewataka wananchi kushirikiana na Polisi kwa kutoa taarifa zinazoashiria uhalifu

Vijana watatu waliotoweka Pemba wapatikana Vijana watatu waliotoweka Pemba wapatikana Reviewed by KUSAGANEWS on April 08, 2018 Rating: 5

No comments: